alumniportal  journals Repository Logo 1   timetable 0 quality a b Staff Mail

HUDUMA ZA MSAADA WA SHERIA

Kamati ya Msaada wa Sheria (LAC) inapenda kuwaarifu wateja wetu kuwa :

 1. Siku ya huduma za msaada wa kisheria ni Ijumaa (SIKU ZA KAZI TU). Huduma huanza saa Nne Asubuhi kila Ijumaa.
 1. Utaratibu wa huduma ni kama ifuatavyo:
 1.  Mteja akifika ataandika jina kwenye karatasi mapokezi.
 2. Huduma zitatolewa kwa aliye fika kwanza (yaani: first come first served) hivyo mteja unashauriwa kuwahi na kuandika jina lako mapema.
 3. Mteja unashauriwa kuja na nakala za nyaraka zote muhimu kuhusiana na suala lako.
 4. Mwanasheria atakaye kuhudumia atakuuliza maswali kadhaa ili kupata taarifa zako na kujaza Fomu Na. 1 na kisha kukufungulia jalada endapo suala lako lina stahiki kupata msaada wa kisheria.
 5. Mwanasheria atakaye kuhudumia akibaini kuwa suala lako linahitaji uwakilishi wa wakili mahakamani atalipeleka suala hilo kwa Mwenyekiti wa kamati, na Mwenyekiti atampangia wakili suala lako.
 6.  Kumuona : Office Na. 8
 7. Barua : Mwenyekiti Kamati ya Msaada wa Sheria
 1.   Kamati haitapokea wateja kutoka Watoa Msaada wa Kisheria (Legal Aid Providers) wengine pasi na kupewa barua ya uthibitisho kuwa mteja ameomba kuhamia hapa kwa sababu mbali mbali.
 2. Ni jukumu la mteja kufuatilia mwenendo wa suala lake. Mteja ukipotea kwa muda mrefu kamati italifunga jalada lako na kuiarifu mahakama (au chombo husika) kuwa  hatukuhudumii tena.
 1. Mteja ana haki ya kupata taarifa ya suala lake kutoka kwa mwanasheria au wakili anaye mhudumia na endapo haridhishwi na taarifa hizo au majibu hayo mteja anayo haki ya kwenda kwa Mwenyekiti wa Kamati (Ofisi No. 8 ), ama kujaza fomu ya malalamiko (inapatikana kwa Mwanasheria, Ofisi No. 1 au Ofisi ya Mwenyekiti).
 1. Mteja anayo haki ya kudai na kupewa jalada/nyaraka zake endapo hahitaji kuendelea kuhudumiwa na LAC. Tafadhali muone Mwenyekiti kwa ajili ya utaratibu wa kurudishiwa jalada.
 1. Kama unahitaji ufafanuzi wa jambo lolote kuhusiana na Kamati ya Msaada wa Sheria tafadali wasiliana na Mwenyekiti kupitia:

                           Chuo Kikuu DSM

                            Dar es Salaam

 1.  Barua Pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
 2. Simu: +255 222 410 463
 3. Ujumbe Mfupi (SMS): 0755 453 639

TAFADHALI ZINGATIA KUWA HUDUMA ZETU NI BURE HAKUNA TOZO/MALIPO YOYOTE. TOA TAARIFA KWA MWENYEKITI ENDAPO UTADAIWA MALIPO YA AINA YOYOTE.

KAMATI YA MSAADA WA SHERIA

CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM 

Welcome note

I am pleased to note that you are a part of the community of the University of Dar-es-Salaam School of Law; as a student, contemplating to become one or an Alumnus.  This webpage provides a synopsis of the courses offered by the School and a variety of activities that the School has been engaged in or about to embark upon.

The School of Law is the oldest legal training institute in the Eastern and Southern African region. The School (then Faculty of Law) was established on Wednesday, 25th October 1961, about three months before the independence of the then Tanganyika to cater for the emerging newly independent States of East Africa, at that time comprising of Kenya, Uganda, Tanganyika and Zanzibar. At its inception, the School was affiliated to the University of London and followed its curriculum.  Despite this affiliation, the focus of its curriculum was designed to cater for local situations that were in line with the aspiration of the newly independent States of the region. From inception, therefore, the School’s role was essentially focused on applied research out of necessity. It had to advise the government in the codification of customary law, integration of court systems and matters of constitution making. 

Read More

Deans’ Message

 

 

 

 

 

 

 

 

The University of Dar es Salaam boasts over 55 years of providing legal education in Tanzania, Read more Deans’ Message

Contact Us

University of Dar es Salaam School of Law.
Deans' Office.
P.o. Box 35093,

Dar es Salaam,
Tanzania.

Email: dean_law@udsm.ac.tz
Landline: +255-(0)22-2410342
Telegram: University of Dar es Salaam.